1 – Quraysh bin Anas amesema:
“Nimemsikia ´Amr bin ´Ubayd akisema: “Siku ya Qiyaamah nitaletwa mbele na kuwekwa mbele ya Allaah. Ataniambia: “Kwa nini ulisema kuwa muuaji yuko Motoni?” Nitajibu: “Wewe ndiye umesema hivo:
وَمَن يَقْتُلْ مُؤْمِنًا مُّتَعَمِّدًا فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِدًا فِيهَا وَغَضِبَ اللَّـهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَابًا عَظِيمًا
“Na yeyote atakayemuua muumini makusudi, basi malipo yake ni Moto ni mwenye kudumishwa humo na Allaah atamghadhibikia na atamlaani na atamuandalia adhabu kuu.”[1]
Ndipo nikamwambia na mimi ndiye nilikuwa mdogo zaidi katika nyumba: ”Unaonaje Akikwambia: ”Mimi nimesema pia:
إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ
“Hakikaha hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.”[2]
Kipi kimekufahamisha ya kuwa mimi sintomsamehe huyu?” Hakusema kitu.”
2 – Ishaaq bin Ibraahiym amehadithia ya kwamba Quraysh bin Anas amesema:
“Nimemuona ‘Amr bin ‘Ubayd baada ya kufariki kwake. Katika ndoto alikuwa amevaa shati nyembamba ambapo ngozi yake ionekane.
Ishaaq amesema:
“Wafasiri wa ndoto wanasema maana yake ni kwamba dini yake ilikuwa nyepesi.”
3 – Mu’aadh bin Mu’aadh amesema:
“Nilikuwa nimekaa na ´Amr bin ‘Ubayd wakati alipomjilia bwana mmoja na kusema: “Ee Abu ‘Uthmaan! Leo nimesikia kufuru!” Akasema: “Usifanye haraka kwa kufuru. Umesikia nini?” Akasema: “Nilimsikia Haashim al-Awqasw akisema: “Aayah:
تَبَّتْ يَدَا أَبِي لَهَبٍ وَتَبَّ
“Imeteketea mikono miwili ya Abu Lahab!”[3]
ذَرْنِي وَمَنْ خَلَقْتُ وَحِيدًا
”Niache Mimi na yule Niliyemuumba pekee.”[4]
hazimo ndani ya ubao Uliohifadhiwa.” Kwani Allaah (Ta´ala) amesema:
وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ
”Naapa kwa Kitabu kinachobainisha. Hakika Sisi tumekifanya kisomeke kwa Kiarabu ili mpate kutia akilini. Hakika hii imo Kwetu katika Mama wa Kitabu imetukuka kwa hakika, imejaa hekima!”[5]
Ukafiri ni nini kama si haya, ee Abu ´Uthmaan?” ´Amr bin ´Ubayd akanyamaza kitambo kidogo. Kisha akamgeukia na kumwambia: “Lau mambo yangelikuwa kama unavyosema, basi Abu Lahab na yule ambaye ameumbwa peke yake wasingelaumiwa.” Ndipo akasema: “Ee Abu ‘Uthmaan! Naapa kwa jina la Allaah hiyo ndiyo dini!”
Mu´aadh bin Mu´aadh amesema:
“Amekuja na kufuru na amerudi na dini yake.”
4 – ´Aaswim al-Ahwal amehadithia ya kwamba amemsikia Qataadah akimsema vibaya ´Amr bin ´Ubayd na akasema:
“Nikapiga magoti na kusema: “Ee Abul-Khattwaab! Inakuweje wanazuoni wanapondana?” Nikaanza kuhisi chuki dhidi ya Qataadah. Ndipo akasema: “Nimemuota ‘Amr alikuwa ameshika Qur-aan na akijaribu kufuta Aayah ndani yake. Ndipo nikamwambia: “Unafanya nini?” Akajibu: “Nataka kuirudisha.” Akaifuta. Ndipo nikasema: “Irudishe!” Akasema: “Siwezi.”
5 – ´Aaswim al-Ahwal amesema:
”Qataadah alikuwa akimsema vibaya ‘Amr bin ‘Ubayd mpaka napiga magoti na kusema: “Ee Abul-Khattwaab! Inakuweje wanazuoni wanapondana?” Akasema: “Ee Ahwal! Mtu amezusha. Afadhali tutaja Bid´ah yake kuliko kuinyamazia. Nikamuota ´Amr… ”
[1] 4:93
[2] 04:116
[3] 111:1
[4] 74:11
[5] 43:2-4
- Muhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy (afk. 385)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Akhbaar ´Amr bin ´Ubayd bin Baab al-Mu´taziliy, uk. 86-91
- Imechapishwa: 16/11/2025

Muhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy (afk. 385)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Akhbaar ´Amr bin ´Ubayd bin Baab al-Mu´taziliy, uk. 86-91
Imechapishwa: 16/11/2025
https://firqatunnajia.com/kwenye-kilele-cha-mutazilah-amr-bin-ubayd/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket