Kwenda msikitini na nguo za kulalia

Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kwenda msikitini kwa mavazi aliolalia?

Jibu: Muhimu mavazi hayo yawe masafi na yenye kusitiri. Yakiwa ni twahara na  masafi swalah inasihi.

Lakini mavazi yenye utata au ambayo yanafanya watu kukuangalia vibaya usiende nayo [msikitini]. Vaa kama wanavyovaa wengine wanapoenda msiktini kuswali.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13389
  • Imechapishwa: 24/06/2020