Kwenda Kuwatembelea Familia Wanaoangalia Chaneli Za Uchawi

Swali: Kipindi cha mwisho tumepewa mtihani kwa kujitokeza chaneli maalum kwa ajili ya uchawi. Wakati mwingine nazikuta kwa baadhi ya ndugu zangu na inaweza kutokea na mimi nikaangalia pasi na kuwaambia kitu. Je, na mimi vilevile naingia ndani ya Hadiyth:

“Atayemwendea kuhani au mpiga ramli basi hatizokubaliwa swalah zake siku arubaini.”?

Pamoja na kuzingatia kwamba haziniathiri. Ni ipi hukumu ya kuziangalia kwa jumla?

Jibu: Kusema kwamba hazikuathiri ni kuitakasa nafsi yako, jambo ambalo halijuzu. Usijiaminishe kuwa hazikuathiri. Haijuzu kwako kukaa pamoja nao. Ima wazifunge na wasiziangalie. Katika hali hiyo unaweza kukaa pamoja nao. Wakikataa na wakaendelea, achana nao na usikae pamoja nao. Jitenge nazo. Usiseme kuwa hazikuathiri kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (06) http://alfawzan.af.org.sa/node/2049
  • Imechapishwa: 03/12/2016