Kwenda katika miji ya kikafiri kutafuta kazi

Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya Hijrah kwenda katika miji ya kikafiri kwa hoja ya kufanya kazi au kuzidisha riziki?

Jibu: Yule mwenye kuhitajia kusafiri kwenda katika miji ya kikafiri kwa ajili ya biashara au kutafuta riziki pamoja na kushikamana na dini yake, hakuna neno kwa hilo ikiwa ana haja ya hilo na katika miji ya Kiislamu hakuna kazi. Lakini maadamu katika miji ya Kiislamu kuna kazi, haijuzu kwake kwenda kwa makafiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-01-13.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014