Basi njia ya kuokoka na hilo ni kuizuia nafsi yako na jambo hilo, kumkubuka Allaah, kuachana na husuda, ujue kwamba ni jambo linalokataliwa juu yako, kwamba ni dhuluma kutoka kwako kwa waja wa Allaah na ni kupinga kwa Allaah (Ta´ala) ambaye ndiye anayewaneemesha waja Wake na ndiye aliyegawa riziki baina ya waja Wake. Basi kuna sababu gani umhusudie fulani kwa sababu Allaah amempa mali, amempa elimu, amempa kazi inayofaa au amempa jambo jingine katika yale aliyoyahalalisha Allaah? Kwa nini umhusudie? Allaah ndiye aliyegawa riziki baina ya waja Wake (Ta´ala). Kufanya hivo ni pingamizi kutoka kwako kwa Mola wako na kuwa na dhana mbaya kutoka kwako kwa Mola wako. Basi muombe Mola wako salama, jihadhari na shari ya nafsi yako, shaytwaan wako na nafsi yako inayoamrisha sana mabaya. Wala usitekeleze husuda yako kwa dhuluma.
Ama anayehusudiwa, basi humdhuru husuda ya mwenye kuhusudu. Hamdhuru isipokuwa akijitahidi kumdhulumu na kumuudhi. Basi ajitetee anapojaribu kumdhulumu kwa maneno, matendo, kumuondoa katika kazi, kumzulia uongo au mfano wa hayo. Basi ashughulikie jambo hilo kwa namna itakayoondoa alichokifanya dhalimu. Imekuja katika Hadiyth:
”Jihadharini na husuda, kwani hula mema kama moto unavyokula kuni.”
Tunamuomba Allaah atulinde.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1928/علاج-الحسد-ومدى-تاثيره
- Imechapishwa: 02/01/2026
Basi njia ya kuokoka na hilo ni kuizuia nafsi yako na jambo hilo, kumkubuka Allaah, kuachana na husuda, ujue kwamba ni jambo linalokataliwa juu yako, kwamba ni dhuluma kutoka kwako kwa waja wa Allaah na ni kupinga kwa Allaah (Ta´ala) ambaye ndiye anayewaneemesha waja Wake na ndiye aliyegawa riziki baina ya waja Wake. Basi kuna sababu gani umhusudie fulani kwa sababu Allaah amempa mali, amempa elimu, amempa kazi inayofaa au amempa jambo jingine katika yale aliyoyahalalisha Allaah? Kwa nini umhusudie? Allaah ndiye aliyegawa riziki baina ya waja Wake (Ta´ala). Kufanya hivo ni pingamizi kutoka kwako kwa Mola wako na kuwa na dhana mbaya kutoka kwako kwa Mola wako. Basi muombe Mola wako salama, jihadhari na shari ya nafsi yako, shaytwaan wako na nafsi yako inayoamrisha sana mabaya. Wala usitekeleze husuda yako kwa dhuluma.
Ama anayehusudiwa, basi humdhuru husuda ya mwenye kuhusudu. Hamdhuru isipokuwa akijitahidi kumdhulumu na kumuudhi. Basi ajitetee anapojaribu kumdhulumu kwa maneno, matendo, kumuondoa katika kazi, kumzulia uongo au mfano wa hayo. Basi ashughulikie jambo hilo kwa namna itakayoondoa alichokifanya dhalimu. Imekuja katika Hadiyth:
”Jihadharini na husuda, kwani hula mema kama moto unavyokula kuni.”
Tunamuomba Allaah atulinde.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1928/علاج-الحسد-ومدى-تاثيره
Imechapishwa: 02/01/2026
https://firqatunnajia.com/kwanini-umhusudu-ndugu-yako/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket