Swali: Baba yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa katika kipindi ambacho kilikuwa kimesheheni ujinga. Ni kwa nini hakupewa udhuru wa ujinga? Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Baba yangu na baba yako wako Motoni.”

Jibu: Kwa sababu watu waliokuwa katika kipindi kabla ya kuja Uislamu walifikiwa na ulinganizi wa Mitume; ulingano wa Ibraahiym na al-Masiyh. Wengi wao walikuwa manaswara na kati yao walikuwemo mayahudi pia. Walifikiwa na ulinganizi wa Mitume. Kwa ajili hiyo iliwasimamia hoja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
  • Imechapishwa: 18/02/2024