Swali: Mwenye kukanusha baadhi ya Sifa au akazipigia mfano anakufuru?

Jibu: Akikanusha Sifa pasina kufuata kichwa mchunga (Taqliyd), ikiwa anawafuata wengine kichwa mchunga na huku anafikiria kuwa hili ndio sahihi, huu ni upotevu lakini hata hivyo hakufurishwi. Anapewa udhuru kwa kufuata kichwa mchunga na ujinga wake. Ama ikiwa ni mwenye kukusudia hilo na huku anajua kuwa hili sio sahihi, lakini akashikamana nalo na kulingania kwalo, huyu anakufuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_03.mp3
  • Imechapishwa: 02/07/2018