Kwanini asikufurishwe anayechukia yaliyotajwa katika Qur-aan au Sunnah?

Swali: Je, ni wajibu kumkufurisha yule mwenye kuchukia kitu kutoka katika Qur-aan au Sunnah za Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na chuki hii iko wazi?

Jibu: Akionyesha chuki waziwazi na akasema kwamba yeye anachukia yale yaliyokuja kutoka kwa Allaah (Ta´ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hapana shaka juu ya ukafiri wake. Ama ikiwa hakuyaanika hayo isipokuwa tu ni jambo liko moyoni mwake, haya hakuna ayajuaye isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall). Lakini akitamka na akasema kuwa yeye anachukia Hadiyth fulani au kwamba anachukia Aayah hii na mfano wa haya, huyu ametamka kufuru waziwazi. Kwa hiyo anahukumiwa kwa mujibu wa aliyotamka kwa ulimi wake. Ama midhali hajatamka basi sisi hakuna tunachoangalia isipokuwa yale ya wazi na hakuna anayejua yaliyomo moyoni isipokuwa Allaah pekee (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Naaqidh-il-Islaam, uk. 123
  • Imechapishwa: 23/11/2018