Kwa kila ambaye anadai kumfuata imaam Abu Haniyfah, Shaafi´iy na Maalik

Wametaja – Abu Haniyfah na wanafunzi zake – ya kwamba ni wenye kuafikiana na madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Hapa kuna Radd kwa wale wanaojinasibisha na Hanafiyyah leo au hapo mwanzoni na wakati huo huo wanaenda kinyuume na Abu Haniyfah katika ´Aqiydah. Katika madhehebu yake wanategemea Fiqh tu na wanaenda kinyume na yeye katika ´Aqiydah. Wanachukua ´Aqiydah ya wanafalsafa na watu wa mantiki.

Kadhalika hili limewapata hata Shaafi´iyyah waliokuja baadae katika wao wanaenda kinyume na Imaam ash-Shaafi´iy katika ´Aqiydah. Wanajinasibisha kwake katika Fiqh tu.

Kadhalika wengi katika Maalikiyyah waliokuja baadae hawako juu ya ´Aqiydah ya Imaam Maalik. Wamechukua madhehebu ya Imaam Maalik katika Fiqh tu, ama kwenye ´Aqiydah ni katika twuruq na watu wa madhehebu ya waliokuja baadae.

Katika ´Aqiydah hii kuna Radd kwa watu hawa na watu mfano wao katika wale ambao wanajinasibisha na maimamu na wanachukua madhehebu ya maimamu wane na wakati huo huo wanaenda kinyume na wao katika ´Aqiydah. Kama mfano wa Ashaa´irah ambao wanajinasibisha na Imaam Abul-Hasan al-Ash´ariy katika madhehebu yake ya kwanza, na wanaacha aliyohakikisha baadae katika madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

Kujinasibisha huku sio sahihi. Kwa sababu lau kweli wangelikuwa katika madhehebu ya maimamu basi wangelikuwa katika ´Aqiydah zao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-it-Twahaawiyyah, Uk. 27-28
  • Imechapishwa: 05/09/2020