Swali: Makhatwiyb wengi wa misikiti katika mwezi huu Khutbah zao zinazungumzia Israa´ na Mi´raaj. Je, kuna ubaya kufanya hivo au hapana?
Jibu: Naona kuwa si jambo la sawa. Kuzungumzia Israa´ na Mi´raaj katika mwezi huu ni kukubaliana na kwamba Israa´ na Mi´raaj ilikuwa katika mwezi huu, jambo ambalo ni la kimakosa. Maoni yaliyo karibu na usawa ni kwamba Mi´raaj ilikuwa katika Rabiy´ al-Awwaal. Kwa sababu Rabiy´ al-Awwaal ndio Wahy ulianza kuteremshwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wahy ulianza kuteremshwa katika Rabiy´ al-Awwaal. Alikuwa akiona ndoto zikija na zikitokea kweli kama alivyoona na Qur-aan imeteremshwa kwake katika Ramadhaan. Maoni yaliyo karibu zaidi na usawa – kwa sababu hakuna andiko la wazi – ni kwamba ni katika Rabiy´ al-Awwaal na si katika Rajab. Kwa ajili hiyo si sawa kwa makhatwiyb kusoma Khutbah za Mi´raaj katika mwezi huu. Kwa sababu mtu kufanya hivo ni kama anathibitisha. Hayo yakikita nyoyoni mwa wasiokuwa na elimu yanakuwa ni kama imani.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (40) http://binothaimeen.net/content/896
- Imechapishwa: 22/08/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)