Kuziwekea mpaka Suurah Aayah na idadi maalum katika Ruqyah

Swali: Nilikuwa nimesibiwa na uchawi. Nikaambiwa na ndugu mmoja nikariri Aayat-ul-Kursiy mara mia, maneno Yake (Ta´ala):

 أَيْنَ مَا تَكُونُواْ يَأْتِ بِكُمُ اللّهُ جَمِيعًا

“Popote mtapokuweko Allaah atakuleteni nyote.” (2:148)

Je, kitendo hichi kimewekwa katika Shari´ah?

Jibu: Muulize dalili juu ya hili. Akikuletea dalili juu ya hili, hakuna neno. Ama ikiwa hakuna dalili, haifai. Kuziwekea mpaka Aayah, Suurah au idadi pasina dalili haikubaliki. Hata hivyo Qur-aan yote ni shifaa na himidi zote ni za Allaah. Qur-aan nzima yote ni shifaa. Kuna baadhi ya Aayah zinakhusishwa katika baadhi ya maradhi. Kama kwa mfano Aayah za uchawi zinakhusishwa kwa uchawi, zinasomwa kwa waliofanyiwa uchawi. Kadhalika Suurat-ul-Faatihah ni Ruqyah, kuna andiko juu ya hilo na Ijmaa´. Kadhalika al-Ikhlaasw, al-Falaq na an-Naas, anasomewa nazo mgonjwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/iglhfn-07-01-1435_0.mp3
  • Imechapishwa: 06/10/2020