Kuzipaka mvi rangi nyeusi iliyochanganywa na hina

Swali: Inajuzu kuzipaka nywele rangi nyeusi kabisa pamoja na hina?

Jibu: Kuzipaka nywele rangi nyeusi kabisa ni haramu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Zibadilisheni mvi hizi na jiepusheni na [rangi] nyeusi.”

Lakini hakuna neno endapo mtu ataichanga pamoja na rangi nyingine na ikawa si nyeusi kabisa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/119-120)
  • Imechapishwa: 28/06/2017