Swali: Mtunzi wa “ar-Rawdhw al-Murbi’” ametaja kwamba ikiwa mwenye kuhiji amekusanya vijiwe vyote katika siku za Tashriyq kisha akaamua kutoka Minaa tarehe 12, basi azike vijiwe vilivyokuwa vimekusudiwa tarehe 13. Je, ni jambo lililowekwa katika Shari´ah?

Jibu: Hayo yanafanywa na wale wasiokuwa wasomi, lakini kitendo hicho hakina msingi. Yasizikwe. Yarushe Minaa. Huenda mtu mwingine akaviokota. Au vilevile unaweza kumpa mtu mwengine avirushe. Ama kuhusu kuvizika ni jambo lisilokuwa na dalili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 19/04/2020