Kuzifanyia kazi fatwa za wanazuoni zilizoko kwenye tovuti?

Swali: Je, inafaa kwangu kuzitendea kazi fatwa zilizopo katika tovuti ya Shaykh Ibn Baaz, tovuti ya Shaykh Ibn ´Uthaymiyn au katika tovuti yenu ikiwa hali yangu inaenda sambamba na yaliyotajwa katika fatwa zenu?

Jibu: Ikiwa una uhakika kweli kuwa fatwa zimetoka kwa hao uliowataja na hali ikawa inaendana sambamba, basi hapana neno. Lakini huhitaji kufanya hivo. Waulize wanazuoni waliopo. Waulize.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 19/05/2023