Kuyatanguliza matamshi ya du´aa na kuyachelewesha mengine

Swali: Vipi kuhusu kuyatanguliza baadhi ya matamshi kabla ya mengine[1]?

Jibu: Haidhuru, jambo ni lenye wasaa.

Hamu ni kwa yale yanayohusiana na masiku yajayo.

Huzuni ni kwa yale yanayohusiana na masiku yaliyopita.

Kushindwa inahusiana na kushindwa kufanya kitu ambacho kunamdhuru kule kushindwa kwake. Hivyo anamwomba Mola wake aweze kukifanya.

Uvivu ni kuhusu yale mambo ambayo anayaweza lakini anaomba aweze kuyafanya kwa sababu ni ya kheri.

Woga na ubakhili ni mambo yanayotambulika. Woga wa kutoweza kuiendea kheri na ubakhili wa kutojitolea mali katika njia zake. Uzito wa deni ni jambo linalotambulika.. Kutenzwa nguvu na watu ni jambo linalotambulika.

[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiomba kwa wingi du´aa hii:

اللّهُـمَّ إِنِّي أَعْوذُ بِكَ مِنَ الهَـمِّ وَالْحُـزْنِ، والعًجْـزِ والكَسَلِ والبُخْـلِ والجُـبْنِ، وضَلْـعِ الـدَّيْنِ وغَلَبَـةِ الرِّجال

”Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokamana na hamu na huzuni, kushindwa na  uvivu, ubakhili na woga, uzito wa deni na kushindwa na watu.” (Tazama “al-Bukhaariy pamoja na al-Fath (11/173). Itakuja katika uk. 89, nambari (137). )

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24298/حكم-مخالفة-الترتيب-في-دعاء-الهم-والحزن
  • Imechapishwa: 25/09/2024