Kuyafukua makaburi ya washirikina kwa ajili ya kujenga msikiti

Swali: Mtu anayetaka kujenga msikiti katika ardhi ambapo akakuta kuna makaburi yasiyo upande wa Qiblah – je, inajuzu kuyafukua makaburi hayo kama alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa makaburi ya washirikina?

Jibu: Hili linaangaliwa. Ikiwa kuna haja, basi litazingatiwa na wenye mamlaka. Iwapo itathibitika kuwa ni makaburi ya makafiri, yataondolewa. Lakini ikiwa ni makaburi ya waislamu, yanaheshimiwa na hubaki pale. Lakini msikiti ujengwe mahali pengine. Ama ikiwa ni makaburi ya makafiri, yataondolewa na msikiti ujengwe mahali hapo, kama alivyofanya Mtume alipofukua na kuyaondoa makaburi ya washirikina.

Swali: Ikiwa ni makaburi ya waislamu yafukuliwe kwa haja?

Jibu: Hapana, hayafukuliwi, hubaki kama yalivyo, yatahifadhiwa na hayaguswi kwa ubaya wowote.

Swali: Hata kwa haja ya kujenga barabara au mfano wake?

Jibu: Dharurah zina hukumu zake, dharurah zina hukumu zake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31120/هل-تنبش-القبور-لبناء-مسجد-او-شق-طريق
  • Imechapishwa: 03/10/2025