Kuweka kokoto au changarawe juu ya kaburi

Swali: Kuweka maji na changarawe ndogondogo juu ya kaburi ni Sunnah? Ni upi mwelekeo wako juu ya Hadiyth ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakataza kuzidisha juu ya ule mchanga uliofukuliwa kwenye kaburi iliopokelewa na Abu Daawuud katika “as-Sunan” yake?

Jibu: Kokoto zinawekwa juu ya kaburi ikiwa kunakhofiwa lisije kusambaratishwa na upepo. Bi maana udongo ule uliowekwa juu ya kaburi usije kupeperushwa. Katika hali hii kunawekwa changarawe ili udongo ukae imara.  Ama kwa mfano wa makaburi yetu tulionayo hii leo udongo hauwezi kupeperushwa na upepo. Katika hali hii hakuna haja ya kuweka kokoto.

Kuhusu Hadiyth maana yake ni pale ambapo hakuna haja ya kufanya hivo. Ama kukiwa kuna haja basi ni lazima kuongeza udongo ili kaburi liweze kuonekana vizuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (31) http://binothaimeen.net/content/707
  • Imechapishwa: 03/11/2017