Swali: Leo kumekithiri maneno mengi juu ya masuala kwamba kuwajaribu watu kwa kutumia watu wengine ni Bid´ah. Ni ipi kanuni juu ya masuala haya?
Jibu: Salaf wamesema kwamba miongoni mwa alama za kujua kuwa mtu ana Bid´ah za Qadariyyah ni watu wa Shaam kumponda al-Awzaa´iy, alama za Jahmiyyah ni kumtukana ´Abdullaah bin Mubaarak na alama za Shiy´ah ni kwamba wanamtukana Sufyaan ath-Thawriy. Imaam Ahmad alikuwa ni mtihani ambao kwao kunapambanuliwa kati ya haki na batili.
Kwa hali yoyote Ahl-ul-Bid´ah wal-Fitnah wana njia mbalimbali ambazo wanatumia kuwaponda na kuwachafua Ahl-us-Sunnah. Wao huwawekea wale viongozi wao vipimo na wanavitumia kuwajaribu Salafiyyuun katika vyuo vikuu, Daar-ul-Hadiyth na kwenginepo kwa majina mbalimbali. Tuachane na watu hawa.
Nikimuona mtu anamtukana Maalik nitilie shaka juu ya Bid´ah yake? Nimwite Salafiy? Nikimuona mtu anarejea kwa Ibn Baaz, Ibn ´Uthaymiyn n.k. tunatambua kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah – Allaah akitaka. Nikitambua mtu miaka na miaka tangu wakati Ibn Baaz yuko hai lakini pamoja na hivyo humuoni akimwendea kamwe, hili linafahamisha nini? Hiki ni kipimo ambacho mtu anapata kumtambua mtu wa haki na mtu wa batili. Alama za mnafiki ni tatu; wakati anapozungumza anasema uongo, anapotoa ahadi anakhalifu na anapoaminiwa anakhini. Alama za waislamu ni kutoleana salamu, kutembeleana n.k. Ukimuona ana vifundo dhidi ya Ahl-us-Sunnah, hawatembelei n.k., haya yanafahamisha nini? Nambie yanafahamisha nini?
- Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Hadm Qawaa´id-il-Mulabbisiyn http://rabee.net/ar/questions.php?cat=26&id=618
- Imechapishwa: 10/03/2018
Swali: Leo kumekithiri maneno mengi juu ya masuala kwamba kuwajaribu watu kwa kutumia watu wengine ni Bid´ah. Ni ipi kanuni juu ya masuala haya?
Jibu: Salaf wamesema kwamba miongoni mwa alama za kujua kuwa mtu ana Bid´ah za Qadariyyah ni watu wa Shaam kumponda al-Awzaa´iy, alama za Jahmiyyah ni kumtukana ´Abdullaah bin Mubaarak na alama za Shiy´ah ni kwamba wanamtukana Sufyaan ath-Thawriy. Imaam Ahmad alikuwa ni mtihani ambao kwao kunapambanuliwa kati ya haki na batili.
Kwa hali yoyote Ahl-ul-Bid´ah wal-Fitnah wana njia mbalimbali ambazo wanatumia kuwaponda na kuwachafua Ahl-us-Sunnah. Wao huwawekea wale viongozi wao vipimo na wanavitumia kuwajaribu Salafiyyuun katika vyuo vikuu, Daar-ul-Hadiyth na kwenginepo kwa majina mbalimbali. Tuachane na watu hawa.
Nikimuona mtu anamtukana Maalik nitilie shaka juu ya Bid´ah yake? Nimwite Salafiy? Nikimuona mtu anarejea kwa Ibn Baaz, Ibn ´Uthaymiyn n.k. tunatambua kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah – Allaah akitaka. Nikitambua mtu miaka na miaka tangu wakati Ibn Baaz yuko hai lakini pamoja na hivyo humuoni akimwendea kamwe, hili linafahamisha nini? Hiki ni kipimo ambacho mtu anapata kumtambua mtu wa haki na mtu wa batili. Alama za mnafiki ni tatu; wakati anapozungumza anasema uongo, anapotoa ahadi anakhalifu na anapoaminiwa anakhini. Alama za waislamu ni kutoleana salamu, kutembeleana n.k. Ukimuona ana vifundo dhidi ya Ahl-us-Sunnah, hawatembelei n.k., haya yanafahamisha nini? Nambie yanafahamisha nini?
Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Hadm Qawaa´id-il-Mulabbisiyn http://rabee.net/ar/questions.php?cat=26&id=618
Imechapishwa: 10/03/2018
https://firqatunnajia.com/kuwatumia-baadhi-ya-wanachuoni-kuwajaribu-watu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)