Kuwatazama mabinamu zako wa kike na kukaa nao

Swali: Je, inafaa kuwatazama mabinamu wa kike licha ya kwamba kaka wapo na baba?

Jibu: Haijuzu kuwatazama. Hata hivyo hapana vibaya kukaa nao muda wa kuwa wamejisitiri na wakati huohuo anainamisha macho mbele ya baba au ndugu zake. Kuhusu kuwatazama haijuzu:

قُل لِّلْمُؤْمِنِينَ يَغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيَحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ

“Waambie waumini wanaume wainamishe macho yao na wahifadhi tupu zao.”[1]

al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanadamu ameandikiwa sehemu ya uzinzi na haiepukiki. Uzinzi wa macho ni kule kuangalia. Uzinzi wa masikio ni kule kusikiliza. Uzinzi wa ulimi ni kule kuongea. Uzinzi wa mkono ni kule kugusa. Uzinzi wa miguu ni kule kutembea. Nafsi inatamani na kutaka na tupu ndio ima inasayadikisha au kuyakadhibisha hayo.”[2]

Muslim amepokea katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Jaabir bin ´Abdillaah (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliyesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa kuhusu mtazamo wa ghafla ambapo akajibu:

“Yageuze macho yako.”

[1] 24:30-31

[2] al-Bukhaariy (6243) na Muslim (2657).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 443-444
  • Imechapishwa: 15/07/2025