Swali: Nimemsikia al-Kabsiy akipendekeza kuwasomea Qur-aan wafu na khaswa makaburini. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
“… mtu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi… ”[1]
Qur-aan imeteremshwa ili iwe ponyo kwa ajili ya miili na mioyo. Hatukufikiwa na khabari yoyote kwamba wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiwasomea wafu. Msichana wake alikufa, ´Uthmaan bin Madh´uun akafariki na wengine wengi pasi na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuamrisha kuwasomea chochote katika Qur-aan.
[1] 53:39
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 174-175
- Imechapishwa: 15/02/2025
Swali: Nimemsikia al-Kabsiy akipendekeza kuwasomea Qur-aan wafu na khaswa makaburini. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَأَن لَّيْسَ لِلْإِنسَانِ إِلَّا مَا سَعَىٰ
“… mtu hatopata [malipo] isipokuwa yale aliyoyafanyia juhudi… ”[1]
Qur-aan imeteremshwa ili iwe ponyo kwa ajili ya miili na mioyo. Hatukufikiwa na khabari yoyote kwamba wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiwasomea wafu. Msichana wake alikufa, ´Uthmaan bin Madh´uun akafariki na wengine wengi pasi na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuamrisha kuwasomea chochote katika Qur-aan.
[1] 53:39
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 174-175
Imechapishwa: 15/02/2025
https://firqatunnajia.com/kuwasomea-qur-aan-wafu/