Swali: Ni ipi hukumu ya yule anayewaficha wale wanaoacha swalah na wanatumia muda wao katika kucheza karata?
Jibu: Ni wajibu juu ya waumini kushirikiana, kama ulivyosikia, kushirikiana katika kheri, kuwapa nasaha wale wanaoacha swalah na kutowaacha katika batili yao pamoja na mashaytwaan. Bali wanawanasihi na kuwaelekeza katika kheri. Ikiwa watasimama sawa ni vyema. Vinginevyo jambo lao lifikishwe kwa wenye mamlaka juu yao ili wasimamie juu yao yale yanayolazimu na ili wafikishwe kwao yale yanayostahiki. Kusudio ni kwamba kuwaacha watu katika batili yao ni jambo la maovu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۚ يَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ
“Waumini wanaume na waumini wanawake ni marafiki wao kwa wao: wanaamrisha mema na wanakataza maovu.”[1]
كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ
“Mmekuwa Ummah bora kabisa ulioteuliwa kwa watu – mnaamrisha mema na mnakataza maovu.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yule miongoni mwenu atakayeona maovu basi ayazuie kwa mkono wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa mdomo wake. Asipoweza, basi afanye hivo kwa moyo wake na hiyo ni imani dhaifu mno.”[3]
Kwa hiyo akijua kwamba watu wa ofisi fulani au nyumba fulani wanapoteza swalah na hawajali, ndugu wanawanasihi, wanawasiliana nao na kuwaelekeza katika kheri. Aidha kuwatahadharisha kutokana na matokeo mabaya ya matendo yao. Ikiwa watanyooka sawa ni vyema. Vinginevyo jambo lao lifikishwe. Ikiwa wako katika idara lifikishwe kwa mkuu wa idara, kwa wenye mamlaka, kwa kiongozi wa kijiji au mfano wa hao ambao inatarajiwa wataleta manufaa katika nafasi hiyo kwa mlango wa kushirikiana katika wema na kumcha Allaah. Afanye hivo baada ya kuwapa nasaha na kujitahidi. Ikiwa itawezekana mwenye kutoa nasaha asiwe peke yake, bali aende na baadhi ya ndugu zake, kwa sababu neno la kundi lina athari zaidi. Ikiwa wanaotoa nasaha ni wawili, watatu au mfano wa hao, basi hilo lina athari kubwa zaidi katika nafsi ya anayenasihiwa na ni karibu zaidi na matokeo mazuri.
[1] 09:71
[2] 03:110
[3] Muslim (49).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3514/حكم-التستر-على-تارك-الصلاة
- Imechapishwa: 26/11/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3514/حكم-التستر-على-تارك-الصلاة
Imechapishwa: 26/11/2026
https://firqatunnajia.com/kuwasitiri-wanaoacha-swalah/