Wanazuoni wamependekeza kufungua kikao cha darsa za Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kukihitimisha kwa kisomo cha msomaji mwenye sauti nzuri ya Qur-aan kwa kadiri itakavyowezekana. Kisha inatakikana kwa msomaji katika hali hizi asome yale yanayofaa kikao na yanayolingana nacho na kwamba kisomo chake kiwe katika Aayah za matumaini na khofu, mawaidha, kuipa kisogo dunia, kuhamasisha Aakhirah, kujiandaa kwa ajili yake, kufupisha matumaini ya dunia na maadili mema.

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 71
  • Imechapishwa: 26/11/2026