Swali: Kuhusu kuwazuia wanawake. Je, inajuzu kuwazuia wanawake?
Jibu: Haijuzu kuwazuia wanawake. Hili ni haramu. Hili ni katika mambo ya kabla ya kuja Uislamu. Kwa maana mtu hataki kumuozesha mwanamke isipokuwa kwa binamu yake au fulani tu. Hili halijuzu. Ikiwa amemchumbia mwanamke mwanaume anayemfaa na kulingana naye, basi aozwe hata kama si wa karibu naye na wala si binamu yake. Hili ni katika matendo ya kipindi kabla ya kuja Uislamu na halijuzu. Haijuzu kuwazuia wanawake kwa kuwafungamanisha na wana wa ami zao. Hili ni jambo ovu. Haijuzu kwa baba wala kwa asiye baba kuwazuia wanawake. Bali pindi anapokuja mwanaume anayefaa, basi waozesheni bila masharti. Hili ndilo jambo la wajibu juu yao.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2133/حكم-الحجر-على-النساء
- Imechapishwa: 02/01/2026
Swali: Kuhusu kuwazuia wanawake. Je, inajuzu kuwazuia wanawake?
Jibu: Haijuzu kuwazuia wanawake. Hili ni haramu. Hili ni katika mambo ya kabla ya kuja Uislamu. Kwa maana mtu hataki kumuozesha mwanamke isipokuwa kwa binamu yake au fulani tu. Hili halijuzu. Ikiwa amemchumbia mwanamke mwanaume anayemfaa na kulingana naye, basi aozwe hata kama si wa karibu naye na wala si binamu yake. Hili ni katika matendo ya kipindi kabla ya kuja Uislamu na halijuzu. Haijuzu kuwazuia wanawake kwa kuwafungamanisha na wana wa ami zao. Hili ni jambo ovu. Haijuzu kwa baba wala kwa asiye baba kuwazuia wanawake. Bali pindi anapokuja mwanaume anayefaa, basi waozesheni bila masharti. Hili ndilo jambo la wajibu juu yao.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2133/حكم-الحجر-على-النساء
Imechapishwa: 02/01/2026
https://firqatunnajia.com/kuwaoza-wanawake-kwa-jamaa-zao-tu/