Swali: Ni ipi hukumu ya kuwaombea du´aa makafiri na wazushi wapate kuongozwa na kutengemaa? Je, kuna maoni tofauti kati ya wanazuoni kuhusu hilo? Ni yepi maoni yenye nguvu juu ya hilo?
Jibu: Uongofu unahitajika na kila mmoja. Kuomba uongofu ni jambo linalotakikana kwa kila mtu; kwa kafiri, mfanya maasi na wengineo. Kila mmoja anahitaji uongofu. Wewe unasoma katika kila Rak´ah:
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ
“Tuongoze njia iliyonyooka.”[1]
Wewe unaomba uongofu hali ya kuwa ni muumini. Maana yake ni kwamba unaomba uthibiti juu ya haki na kuongezewa uongofu. Kwa hiyo kila mmoja ni mhitaji wa uongofu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema wakati alipoambiwa kuwa kabila la Daws limekufuru na kuasi:
”Ee Allaah waongoze Daws na walete kwangu. Ee Allaah waongoze Daws na walete kwangu.”
Aliwaombea du´aa wengi katika makafiri na Allaah akawaongoza. Ikiwa kafiri au mfanya maasi ni dhalimu mwenye kuwadhuru watu, inajuzu pia kumuombea du´aa ya maangamivu. Inajuzu kuomba aongoke na inajuzu kuomba aangamie. Yote mawili yanafaa. Lakini khaswa wanapowasumbua na kuwadhuru watu, katika hali hiyo ni wenye kustahiki zaidi kuombewa du´aa ya maangamivu kwa sababu ya kuwa kwao mbali na uongofu. Ikiwa wamejizuilia na shari zao wenyewe, basi wanaombewa uongofu kwamba Allaah awaongoze katika haki na kwamba awafungue macho yao.
[1] 1:6
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30949/حكم-الدعاء-للكفار-والمبتدعة-بالهداية-والصلاح
- Imechapishwa: 16/09/2025
Swali: Ni ipi hukumu ya kuwaombea du´aa makafiri na wazushi wapate kuongozwa na kutengemaa? Je, kuna maoni tofauti kati ya wanazuoni kuhusu hilo? Ni yepi maoni yenye nguvu juu ya hilo?
Jibu: Uongofu unahitajika na kila mmoja. Kuomba uongofu ni jambo linalotakikana kwa kila mtu; kwa kafiri, mfanya maasi na wengineo. Kila mmoja anahitaji uongofu. Wewe unasoma katika kila Rak´ah:
اهْدِنَا الصِّرَاطَ الْمُسْتَقِيمَ
“Tuongoze njia iliyonyooka.”[1]
Wewe unaomba uongofu hali ya kuwa ni muumini. Maana yake ni kwamba unaomba uthibiti juu ya haki na kuongezewa uongofu. Kwa hiyo kila mmoja ni mhitaji wa uongofu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema wakati alipoambiwa kuwa kabila la Daws limekufuru na kuasi:
”Ee Allaah waongoze Daws na walete kwangu. Ee Allaah waongoze Daws na walete kwangu.”
Aliwaombea du´aa wengi katika makafiri na Allaah akawaongoza. Ikiwa kafiri au mfanya maasi ni dhalimu mwenye kuwadhuru watu, inajuzu pia kumuombea du´aa ya maangamivu. Inajuzu kuomba aongoke na inajuzu kuomba aangamie. Yote mawili yanafaa. Lakini khaswa wanapowasumbua na kuwadhuru watu, katika hali hiyo ni wenye kustahiki zaidi kuombewa du´aa ya maangamivu kwa sababu ya kuwa kwao mbali na uongofu. Ikiwa wamejizuilia na shari zao wenyewe, basi wanaombewa uongofu kwamba Allaah awaongoze katika haki na kwamba awafungue macho yao.
[1] 1:6
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30949/حكم-الدعاء-للكفار-والمبتدعة-بالهداية-والصلاح
Imechapishwa: 16/09/2025
https://firqatunnajia.com/kuwaombea-duaa-makafiri-na-ahl-ul-bidah/