Swali: Haifai kukaa na wanajeshi wa kinaswara kwa ajili ya kuwalingania katika Uislamu?
Jibu: Mayahudi pia. Wote wawili mayahudi na manaswara wanalinganiwa katika Uislamu.
Swali: Nakusudia wakati wakiwa huru wanakaa kwenye viti na pombe inasambazwa kati yao. Je, walinganiwe au waachwe?
Jibu: Awaendee ikiwa hakuna wakati mwingine isipokuwa huu na awabainishie kuwa Allaah amewaumba kwa ajili ya ´ibaadah, kwamba Allaah amewawajibishia kumfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwamba yeye ndiye Nabii wa mwisho, kwamba Allaah amewaharamishia pombe na amewaharamishia uzinzi. Hii ndio dini ya Uislamu. Lakini kitu cha kwanza awalinganie katika kumwabudu Allaah pekee kwanza na kumfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile awabainishie miongoni mwa mazuri ya Uislamu ni uharamu wa maovu hayo wayafanyayo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24536/حكم-دعوة-المشركين-للاسلام-وهم-بمجلس-خمر
- Imechapishwa: 26/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)