Kuwakilisha mtu akurushie vijiwe katika Hajj

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu aliyemwakilisha mwingine vijiwe ilihali anahiji Hijjah ya faradhi?

Jibu: Iwapo ana udhuru wa kushindwa kupiga vijiwe mwenyewe, kama ugonjwa, udogo wa umri, udhaifu wa mwili au akiwa ni mwanamke asiyeweza kustahimili msongamano, akiwa mgonjwa, mjamzito au mfano wa udhuru kama huo, basi uwakilishi wake ni sahihi. Ama akiwa na nguvu na hana udhuru wowote, basi uwakilishi haukubaliki. Bali anapaswa kupiga vijiwe mwenyewe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1964/حكم-التوكيل-في-الرمي-في-الحج
  • Imechapishwa: 02/01/2026