Swali: Ni ipi hukumu ya kuleta maji makaburini na kuwapa wale waliohudhuria?

Jibu: al-Lajnah ad-Daaimah wamefutu kwamba kitendo hicho hakitakikani. Kwani hiyo ni njia kwa baadhi ya watu wakathibitisha hilo na wakachukulia kuwa ni Sunnah. Kwa hiyo haitakikani kutoa maji makaburini. Kuzika wakati wake ni mfupi. Mtu anatakiwa kufanya subira au awe na maji yake. Ama kitendo cha watu kupewa maji, swadaqah na baadhi ya watu wanaweza kwenda mbali zaidi ambapo wakatoa tufaha au kitu kingine. Watu wanaweza kuchukulia kuwa kitendo hicho ni Sunnah au kimependekezwa. Kwa hiyo kuacha kufanya hivo ndio bora zaidi. Hii ndio fatwa ya al-Lajnah ad-Daaimah inayokataza kitendo hichi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 20/02/2021