Kuwaendea wanajimu na kuwasadikisha

Swali: Vipi kuwaendea wanajimu na kuwasadikisha?

Jibu: Hili linahusiana na wapiga ramli. Haijuzu kuwaendea wapiga ramli. Ni moja katika madhambi makubwa. Akiwasadikisha anakufuru. Tunamuomba Allaah usalama. Haijuzu kuwauliza ingawa hawakusadikisha. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayemwendea mpiga ramli na akamuuliza juu ya kitu, basi hazitokubaliwa swalah zake nyusiku arobaini.”

Hata asipowasadikisha. Tunamuomba Allaah usalama. Kitendo hicho kinapelekea kusema kutambua elimu iliyofichikana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23926/حكم-الذهاب-للمنجمين-وتصديقهم
  • Imechapishwa: 01/06/2024