Kuwabusu mabinamu wa kike na kupeana nao mikono

Swali: Mimi nina binamu yangu wa kike ambaye amefikisha miaka sabini. Je, inafaa kumbusu kichwa chake juu ya Hijaab yake au kusalimiana naye kwa kupeana mkono kutokana na uzee wake?

Jibu: Haifai kwako kusalimiana naye kwa kupeana mkono wala kumbusu kichwa chake wala mwenginewe. Bali kilichowekwa katika Shari´ah ni kusaliama naye kwa maneno peke yake ingawa atakuwa kikongwe. Kwa sababu sio Mahram yako. Hakuna neno ukamuuliza hali yake na hali ya watoto wake na mfano wa hayo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mimi sipeani mikono na wanawake.”

Wanaingia wazee pia na wengine. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Naapa kwa Allaah mkono wa Mtume wa Allaah haukupatapo hata siku moja kugusa mkono wa mwanamke. Walikuwa wakila kiapo kwake kwa maneno peke yake.”

Bi maana wanawake wasiokuwa Mahram zake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (07/183)
  • Imechapishwa: 13/06/2021