Kuwaalika watu chakula na kufanya kisomo kwa ajili ya maiti

Swali: Baadhi ya watu wanawaalika watu chakula na wanawalazimisha kumsomea maiti Suurah ”al-Ikhlaasw”?

Jibu: Haina msingi wowote. Haina msingi wowote. Hakuna suala la kutengeneza chakula wala kusoma. Ama wakitengenezewa chakula na majirani zao au majirani wakawaletea zawadi, hilo ni zuri. Kama alivyowaamrisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) familia yake wawapelekee chakula watu wa Ja´far alipofariki, kwa sababu limewapata lililowashughulisha. Majirani wa maiti wakileta chakula cha jioni au cha mchana kwa familia ya maiti, hilo ni zuri. Lakini familia ya maiti kuandalia watu chakula na kuwakaribisha kwa sababu ya msiba, hapana. Hilo ni miongoni mwa matendo ya kipindi kabla ya kuja Uislamu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28497/حكم-الدعوة-لطعام-مع-قراءة-الاخلاص-للميت
  • Imechapishwa: 20/04/2025