Kuvaa nguo mpaka nusu muundi ni kutafuta umaarufu?

Swali: Anayesema kwamba kuvaa nguo mpaka nusu muundi hii leo ni katika kutafuta umaarufu?

Jibu: Hapana, ni kosa. Inafaa kuvaa mpaka nusu muundi. Bali kwa mujibu wa kikosi cha wanazuoni ndio bora zaidi. Isipokuwa ikiwa inapelekea katika majambo, katika hali hiyo aiteremshe mpaka juu ya mafundo ya miguu. Asijitie katika mambo yatayomdhuru. Kuvaa mpaka nusu muundi na mpaka juu ya vifundo vya miguu yote yanafaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24085/هل-يعد-اللبس-الى-نصف-الساقين-من-الشهرة
  • Imechapishwa: 25/08/2024