Swali: Je, kuvaa kilemba ni Sunnah?

Jibu: Kilemba kilikuwa ni katika desturi za waarabu. Wanazuoni wengi wanaona kwamba mavazi hayaingii moja kwa moja katika masuala ya Sunnah na Bid’ah kwa kuwa ni mambo yanayohusiana na mila na desturi. Kwa hiyo hapana neno kukivaa, na pia hapana vibaya kutokivaa. Ni katika mila za waarabu kabla ya Shari´ah ya Kiislamu.

Swali: Je, inaweza kusemwa kuwa ni Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24727/هل-لبس-العمامة-سنة
  • Imechapishwa: 03/12/2024