Kuuza nyama ya wanyama kwa kutumia wanyama mwingine

Swali: Je, inajuzu ribaa ya kuchelewesha kwa kuuza nyama kwa mnyama asiye wa jinsia yake?

Jibu: Hakuna ubaya. Kuuza nyama kwa mnyama hakuna tatizo. Huyu ni mnyama tofauti, ni kitu kilichojitegemea. Hapa ribaa haihusiki pamoja na kitu kingine. Akikinunua kondoo kwa ngamia au kwa kitu cha nyama ya kondoo au ya ng’ombe, hakuna tatizo. Hilo haliingii katika ribaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1480/حكم-بيع-اللحم-بحيوان-غيره-نسيىة
  • Imechapishwa: 21/12/2025