Swali: Je, inajuzu kufanya biashara ya mbwa wa uwindaji?

Jibu: Hapana, mbwa hauuzwi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuuza mbwa na akasema:

”Thamani ya mbwa ni najisi.”

Lakini anaweza kumlea tu na kumfundisha.

Swali: Je, mtu anatakiwa kulipa fidia ya thamani yake?

Jibu: Hapana, hakuna fidia wala kitu chochote, kwani hana thamani.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25326/ما-حكم-التجارة-في-كلاب-الصيد
  • Imechapishwa: 28/02/2025