Swali: Vipi kuhusu ambaye amesema kuwa inajuzu kuuza deni kwa deni, lakini kwa sharti la kupokea malipo kabla ya kuachana kwenye kikao?

Jibu: Hili halina tatizo, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna tatizo kuchukua kwa bei ya siku hiyo.”

Deni kwa deni linakuwa lote limecheleweshwa.

Swali: Vipi ikiwa limecheleweshwa?

Jibu: Hapana. Lakini ikiwa deni linabadilishwa kwa kitu kinacholipwa papohapo, basi hilo halihesabiwi kuwa deni.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25392/ما-حكم-بيع-الدين-بالدين
  • Imechapishwa: 08/03/2025