Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak katikati ya darsa na wakati wa kumuitikia muadhini?
Jibu: Hakuna neno. Kilichokatazwa ni kutumia Siwaak ndani ya swalah na wakati wa kusikiliza Khutbah. Ni lazima kusikiliza Khutbah ya ijumaa na wala mtu asizungumze kama ambavyo vilevile hatakiwi kuzungumza wakati wa swalah, asimuitikia mwenye kumsalimia kwa mkono wala mwenye kuchemua. Ama wakati wa darsa na wakati wa adhaana hakuna neno.
Pengine mtu akauliza kama inafaa kwake kuitikia “Aamiyn” wakati wa Khutbah ya ijumaa au kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Ndio, hakuna neno. Afanye hivo kati yake yeye na nafsi yake aitikie “Aamiyn” na amswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu haya sio maneno ya watu. Kilichokatazwa ni maneno ya watu. Kadhalika asiguseguse vijiwe, asicheze wakati wa Khutbah na wala asitumie Siwaak. Wala asimtakie rehema mwenye kuchemua na wala asiitikie salamu.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
- Imechapishwa: 19/10/2019
Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak katikati ya darsa na wakati wa kumuitikia muadhini?
Jibu: Hakuna neno. Kilichokatazwa ni kutumia Siwaak ndani ya swalah na wakati wa kusikiliza Khutbah. Ni lazima kusikiliza Khutbah ya ijumaa na wala mtu asizungumze kama ambavyo vilevile hatakiwi kuzungumza wakati wa swalah, asimuitikia mwenye kumsalimia kwa mkono wala mwenye kuchemua. Ama wakati wa darsa na wakati wa adhaana hakuna neno.
Pengine mtu akauliza kama inafaa kwake kuitikia “Aamiyn” wakati wa Khutbah ya ijumaa au kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Ndio, hakuna neno. Afanye hivo kati yake yeye na nafsi yake aitikie “Aamiyn” na amswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu haya sio maneno ya watu. Kilichokatazwa ni maneno ya watu. Kadhalika asiguseguse vijiwe, asicheze wakati wa Khutbah na wala asitumie Siwaak. Wala asimtakie rehema mwenye kuchemua na wala asiitikie salamu.
Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (13) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191589#219913
Imechapishwa: 19/10/2019
https://firqatunnajia.com/kutumia-siwaak-kuitikia-salamu-na-kumswalia-mtume-wakati-wa-khutbah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)