Swali: Leo kunaongelewa sana kuhusu mada ya Ruqyah. Baadhi ya watu wanachukulia sahali na wengine wanakazia. Baadhi ya watu wanafanya Ruqyah kwa yanayoafikiana na Sunnah na wengine wanafanya kwa Ijtihaad zao. Na ipi nasaha yako kwa wale wanaojishughulisha na Ruqyah?
Jibu: Leo Ruqyah inafanywa kwa kutafuta pesa. Wamejiingiza katika hili wasiyoistahiki. Wanafanya hivyo kwa kutafuta pesa. Hali kadhalika, wamejishughulisha nayo watu ambao ´Aqiydah zao ni mbovu kwa kutafuta pesa. Na kuna watu wamejiingiza kwayo wanaichanganya (Ruqyah hiyo) na mambo ya kishirki na hirizi. Yote haya yanafanywa kwa ajili ya kutafuta pesa. Leo Ruqyah imekuwa ni riziki na biashara. Na hili ni jambo halijuzu. Haijuzu isipokuwa kwa mtu ambaye ni mjuzi wa Ruqyah, mwenye ´Aqiydah nzuri na anataka kihakika kumnufaisha ndugu yake na si kwamba anachotaka yeye ni pesa tu. Lengo lake ni kutaka kumnufaisha ndugu yake mgonjwa. Na ikitokea akapewa kitu katika mali, haina neno akakichukua.
Ama kuichukulia kuwa ndio riziki kwa kufungua maduka, huku ni kuchupa mipaka kwa Ruqyah na ni jambo linalofanywa kwa kutaka (kulenga) pesa tu na si kutaka kuwanufaisha watu, Kunaweza kupenyeza ndani yake – kama tulivyosema – wanganga na wachawi na wakasoma katika vitabu vya kiganga, wakawasomea watu ili wachume pesa. Kwa kuwa kuna vitabu vya kiganga kwa [kutumia] jina la Ruqyah. Ndani yavyo kuna uchawi, shari, kutafuta kinga kwa majini na Mashaytwaan, kuna utafutaji msaada kwa asiyekuwa Allaah (´Azza wa Jalla). Ni lazima mwenye kufanya Ruqyah awe ni mtu mwenye elimu, Baswiyrah, kuaminika na awe na ´Aqiydah nzuri.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=cHdTE5Brz3c
- Imechapishwa: 23/03/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related

Bid´ah zimezozoeleka atika Ruqyah
https://www.youtube.com/watch?v=rv-4tVKEdHA Katika zama hizi, watu wameendelea katika suala la Ruqyah nawameichukulia kuwa riziki na biashara. Wakafungua maduka ya kufanya Ruqyah. Kama ofisi za madaktari. Na wanaichukulia (hiyo Ruqyah) pesa kama wanavyofanya madaktari. Mambo kama haya kunakhofiwa juu yake maangamivu. Kwa kuwa lengo lao ni kuchuma pesa. Na pengine wasijali Halali…
In "´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan"
Kuacha swalah ya mkusanyiko msikitini kwa sababu ya Ruqyah
Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kushughulika na kuwasomea watu Ruqyah na hivyo akaacha swalah ya mkusanyiko msikitini? Jibu: Hili ni kosa kubwa. Haijuzu kwa chochote kumshughulisha na swalah, sawa ikiwa ni Ruqyah au kitu kingine. Huu sio udhuru kwa kuacha swalah ya mkusanyiko msikitini. Anaweza kurudi na kuendelea kusoma Ruqyah.…
In "Hukumu ya swalah ya mkusanyiko"
Hali za wengi wenye kujishughulisha na Ruqyah
Swali: Je, mtu yeyote anaweza kumsomea mwingine Ruqyah au hili ni jambo kwa watu maalum tu? Jibu: Anatakiwa ajue hukumu za Ruqyhah. Ni lazima awe anajua hukumu za Ruqyah na yenye kujuzu na yasiyojuzu. Baadhi yao wanasoma kwenye vitabu vya makhurafi na wanakuja na kuwasomea navyo watu ili waweze kupata pesa.…
In "Ruqyah - Matabano"