Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia manukato yanayojulikana kama “cologne” ambayo yanatambulika kuwa na alcohol?

Jibu: Manukato yanayojulikana kuwa yana pombe ya kulevya hayatumiki, kama vile “kologne”. Wamehadithia madaktari wengi kwamba hayakosi kuwa na kilevi na kwamba huwa yanatofautiana kiwango chake; baadhi yake 80%, baadhi 60%, baadhi 40% na kadhalika. Hivyo haifai kuyatumia. Ingawa baadhi ya watu wametia wepesi na wakayatumia. Hata hivyo nasaha yangu kwa mwanafunzi ni kwamba asiyatumie manukato hayo. Manukato ya cologne yanatambulika kuwa yana spirit, nacho ni kileo.

Kuhusu manukato mengine siyajui. Lakini ikijulikana kuwa yana kitu cha kulevya na kwamba kiasi chake kikubwa kinalevya, basi usiyatumie. Bali tumia manukato yanayojulikana na mafuta ya waridi, mafuta ya amberi, mafuta ya udi yanayojulikana ambayo hayana kitu cha kulevya.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30116/ما-حكم-استعمال-العطورالتي-فيها-كحول
  • Imechapishwa: 11/09/2025