Swali: Kasiri za sherehe za harusi hupatikana ndani yake baadhi ya maovu. Je, inawapasa wanafunzi wa elimu kuzitembelea, kuwapa mawaidha, kuwaelekeza na kuwabainishia?
Jibu: Wanatakiwa kutumia fursa hii. Walinganizi na wanafunzi wazitembelee kasiri hizi wakati wa mkusanyiko na wawapelekee nasaha na maelekezo kutokana na mkusanyiko unaokusanya kundi kubwa la wajinga na wanafunzi miongoni mwa wanawake na wanaume. Kutumia fursa hii kwa maelekezo, maonyo na nasaha ni jambo linalotakiwa. Inawapasa wanazuoni, khaswa walinganizi wanaolingania kwa Allaah, wahudhurie, waonye, wawaidhi na wakumbushe. Vivyo hivyo mikusanyiko mingine na mikutano mingine yote ikiwa itawezekana hilo, basi hilo lina kheri kubwa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29383/كيف-يكون-النصح-والانكار-بقصور-الافراح
- Imechapishwa: 05/08/2025
Swali: Kasiri za sherehe za harusi hupatikana ndani yake baadhi ya maovu. Je, inawapasa wanafunzi wa elimu kuzitembelea, kuwapa mawaidha, kuwaelekeza na kuwabainishia?
Jibu: Wanatakiwa kutumia fursa hii. Walinganizi na wanafunzi wazitembelee kasiri hizi wakati wa mkusanyiko na wawapelekee nasaha na maelekezo kutokana na mkusanyiko unaokusanya kundi kubwa la wajinga na wanafunzi miongoni mwa wanawake na wanaume. Kutumia fursa hii kwa maelekezo, maonyo na nasaha ni jambo linalotakiwa. Inawapasa wanazuoni, khaswa walinganizi wanaolingania kwa Allaah, wahudhurie, waonye, wawaidhi na wakumbushe. Vivyo hivyo mikusanyiko mingine na mikutano mingine yote ikiwa itawezekana hilo, basi hilo lina kheri kubwa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29383/كيف-يكون-النصح-والانكار-بقصور-الافراح
Imechapishwa: 05/08/2025
https://firqatunnajia.com/kutumia-fursa-ya-mikusanyiko-yenye-maovu-kwenda-kukemea-maovu/