Swali: Je, mtu ambaye ametumbukia ndani ya uzinzi kisha akatubu na baadaye akajisalimisha katika mahakama yasiyohukumu kwa hukumu ya Uislamu?

Jibu: Namshauri atubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Wanazuoni wamekinzana kama anatakiwa kujisalimisha mwenyewe ili aadhibiwe au bora kwake ni yeye ajisitiri na dhambi yake. Kinachodhihiri ni kwamba bora ni yeye kujisitiri na dhambi yake. Kisa cha Maa´iz kinatambulika pale ambapo alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akakiri dhambi yake ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:

“Umekunywa pombe? Pengine umembusu peke yake.” Maa´iz akasema hapana ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Umemjamii?” Akajibu: “Ndio.” Hapo ndipo akaadhibiwa.”

Vile ninavoona ni kuwa bora ni yeye kujisitiri kwa dhambi yake na asiende mahakamani.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 246
  • Imechapishwa: 02/04/2025