Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
فَمَن جَاءَهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىٰ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللَّـهِ
“Yule atakayefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake ambapo akakoma, basi ni yake yale yaliyopita na jambo lake iko kwa Allaah.”[1]
Aayah hii inamuhusu mtu ambaye alikuwa hajui na akakusanya pesa nyingi zinazotokana na ribaa kisha baadaye akatubu. Udhahiri wa Aayah ni kuwa atabaki na pesa zote alizochuma na hakuna kinachomlazimu isipokuwa tu ktuubu, kwa sababu alikuwa ni mjinga. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema tena:
وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُءُوسُ أَمْوَالِكُمْ لَا تَظْلِمُونَ وَلَا تُظْلَمُونَ
”Mkitubu basi mtapata rasilimali zenu – msidhulumu na wala msidhulumiwe.”[2]
Aayah hii inamuhusu yule mtu ambaye alikula ribaa kwa makusudi na baadaye akatubu. Anatakiwa kubaki na ile rasilimali yake tu na asichukue ile ziada. Tofauti kati ya watu hawa wawili ni kwamba yule wa kwanza alikuwa akila ribaa na huku hajui, akapata pesa nyingi na baadaye akatubu – hakuna kinachomlazimu isipokuwa tu kutubu. Aayah ya pili alikuwa akila ribaa [kwa kujua] na baadaye akatubu – huyu anatakiwa kuchukua tu ile rasilimali yake.
[1] 2:275
[2] 2:279
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 277-278
- Imechapishwa: 27/05/2025
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket