Kutokwa na damu mapuani baada ya kutawadha

Swali: Nikitokwa na damu mapuani baada ya kutawadha nalazimika kurudi kutawadha upya?

Jibu: Ikiwa ndogo haidhuru. Ikiwa nyingi basi lililo salama zaidi mtu atawadhe. Kwa sababu wanachuoni wengi wa Fiqh wanaona kuwa damu nyingi inachengu wudhuu´. Lakini hata hivyo ni jambo halina dalili za wazi. Lililo salama zaidi kwa muislamu atawadhe tena upya kwa ajili ya kutoka ndani ya tofauti. Kwa ajili hii ndio maana al-Bukhaariy ametenga mlango ukisema: Wale wenye kuonelea kuwa wudhuu´ hauchenguki isipokuwa kwa kutokwa na kitu kwenye tupu ya mbele au ya nyuma. Kwa hiyo mtu akitokwa na damu nyingi lililo salama zaidi kwake atawadhe. Ama damu ndogo, kama tone moja, mbili n.k., hakuna neno.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 22/07/2018