Kutokea upande gani maiti ashushwe ndani ya kaburi?

Swali: Kutokea upande gani maiti anatakiwa kushushwa ndani ya kaburi?

Jibu: Kutokea upande ule ambao ni rahisi. Baadhi ya wanachuoni wanasema kwamba ashushwe kutokea upande wa miguu yake. Wanachuoni wengine wanasema ashushwe kutokea upande wa kichwa chake. Jambo hili lina wasaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/181)
  • Imechapishwa: 01/09/2021