Swali: Je, inafaa kutoka msikitini baada ya adhaana kuliendea jambo la wajibu, kama mfano wa kumwamsha aliyelala? Ni ipi hukumu ya kuufanya msikiti kuwa ni njia ya watu kupita?
Jibu: Hapana vibaya kutoka msikitini kwa sababu ya udhuru, kama vile kumwamsha mwenye kulala na mfano wake, kwa sharti arudi kabla hakujakimiwa swalah. Vivyo hivyo ambaye amemwamrishwa kutoka na baba yake kwa sababu ya haja fulani na anaweza kurejea kabla ya kuanza kuswaliwa swalah ya mkusanyiko.
Hata hivyo haitakikani kuufanya msikiti ni njia ya watu kupita isipokuwa kukiwa kuna haja. Misikiti imejengwa kwa ajili ya swalah, kisomo cha Qur-aan na Dhikr. Lakini inajuzu kupita msikitini ikiwa kuna haja, kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا
“… wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho.”[1]
[1] 4:43
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/201)
Swali: Je, inafaa kutoka msikitini baada ya adhaana kuliendea jambo la wajibu, kama mfano wa kumwamsha aliyelala? Ni ipi hukumu ya kuufanya msikiti kuwa ni njia ya watu kupita?
Jibu: Hapana vibaya kutoka msikitini kwa sababu ya udhuru, kama vile kumwamsha mwenye kulala na mfano wake, kwa sharti arudi kabla hakujakimiwa swalah. Vivyo hivyo ambaye amemwamrishwa kutoka na baba yake kwa sababu ya haja fulani na anaweza kurejea kabla ya kuanza kuswaliwa swalah ya mkusanyiko.
Hata hivyo haitakikani kuufanya msikiti ni njia ya watu kupita isipokuwa kukiwa kuna haja. Misikiti imejengwa kwa ajili ya swalah, kisomo cha Qur-aan na Dhikr. Lakini inajuzu kupita msikitini ikiwa kuna haja, kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:
وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا
“… wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho.”[1]
[1] 4:43
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/201)
https://firqatunnajia.com/kutoka-msikitini-baada-ya-kuadhiniwa/