Kuwa chini ya uongozi wa mtawala wa Kiislamu, haijalishi kitu mapungufu atayokuwa nayo, maasi, dhuluma na unyanyasaji, ni rehema na usalama kwa watu. Kukiwepo mtawala watu wanaweza kutafuta riziki zao na kutafuta elimu kwa usalama na amani. Watu hawachelei juu ya mali zao, hesima zao wala damu zao. Mambo huwa hivi hata kama mtawala atakuwa mwenye kudhulumu huhisi amani kutokana na uwepo wake.
Allaah amrehemu Imaam Ibn Taymiyyah ambaye amesema kwamba kuwa na mtawala dhalimu kwa miaka sitini ni bora kuliko siku moja pasi na mtawala. Watu kuishi miaka sitini chini ya uongozi wa mtawala mkandamizi ambaye anawadhulumu, anawapiga na anawanyima haki zao lakini hata hivyo kuna amani na usalama ndani ya nchi, ni bora kuliko siku moja bila mtawala. Sahihi, kwa sababu anapokuwepo mtawala kunakuwa hakuna machafuko.
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 112-113
- Imechapishwa: 13/05/2026
Kuwa chini ya uongozi wa mtawala wa Kiislamu, haijalishi kitu mapungufu atayokuwa nayo, maasi, dhuluma na unyanyasaji, ni rehema na usalama kwa watu. Kukiwepo mtawala watu wanaweza kutafuta riziki zao na kutafuta elimu kwa usalama na amani. Watu hawachelei juu ya mali zao, hesima zao wala damu zao. Mambo huwa hivi hata kama mtawala atakuwa mwenye kudhulumu huhisi amani kutokana na uwepo wake.
Allaah amrehemu Imaam Ibn Taymiyyah ambaye amesema kwamba kuwa na mtawala dhalimu kwa miaka sitini ni bora kuliko siku moja pasi na mtawala. Watu kuishi miaka sitini chini ya uongozi wa mtawala mkandamizi ambaye anawadhulumu, anawapiga na anawanyima haki zao lakini hata hivyo kuna amani na usalama ndani ya nchi, ni bora kuliko siku moja bila mtawala. Sahihi, kwa sababu anapokuwepo mtawala kunakuwa hakuna machafuko.
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 112-113
Imechapishwa: 13/05/2026
https://firqatunnajia.com/42-bora-watawala-madhalimu-kuliko-kukosekana-watawala-kabisa/