Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

Viongozi na kiongozi wa waumini wanatakiwa kusikilizwa na kutiiwa sawa wawe wema au waovu. Yule mwenye kuchukua ukhaliyfah, watu wakakusanyika juu yake na wakaridhika nao na yule mwenye kuchukua uongozi kwa mabavu mpaka akawa khaliyfah anaitwa kiongozi wa waumini.

MAELEZO

Hii ndio ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Namna hii ndivo wanavotaamiliana na watawala, ni mamoja ni watawala wa ngazi ya juu kabisa katika nchi, kama walivyokuwa makhaliyfah mwanzoni mwa Uislamu, au ni wakuu wa mikoa. Hawa ni viongozi wa waumini na wakuu wa mikoa hii. Ni lazima kwa raia wote kuwatii katika yale ambayo ni mema. Ni lazima kuwasaidia katika kila kheri na kuwaombea du´aa kwa siri na hadharani. Ni haramu kufanya uasi dhidi yao. Amri zao kkatika yaliyo mema zinatakiwa kutekelezwa katika hali zote. Raia wanapaswa kujihadhari kuwakhalifu na kwenda kinyume nao, kwa sababu jambo hilo linafarikisha umoja wa waislamu na kusababisha vurugu, zinavunjwa heshima, umwagikaji wa damu na wizi. Watu watageukiana wao kwa wao, kama inavyotambulika. Tunasikia matukio mbalimbali ya mapinduzi, kupinduliwa kwa magavana na mfano wa matukio kama hayo, mambo yasiyo na hekima. Matokeo yake ni wizi, mauaji na vurugu. Anauliwa ambaye ni mnyonge, mali yake inaibiwa na kuvunjwa heshima yake. Kwa sababu ya majaribio ya mapinduzi kunatokea machafuko.

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 112
  • Imechapishwa: 13/05/2026