Kila ambaye atafuata njia ya watu hawa wema ni miongoni mwao na atafufuliwa pamoja nao siku ya Qiyaamah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtu atakuwa pamoja na yule anayempenda.”[1]
Yule anayempenda Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake watukufu na maimamu wa elimu katike vile vizazi vyema atafufuliwa pamoja nao. Nawapongeza wale wanaofuata ´Aqiydah na Shari´ah ya Mtume mteule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na amekula khasa yule mwenye kwenda kinyume na Sunnah na Ahl-us-Sunnah!
Haitoshi kudai tu kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na wale waliokuja baada yao. Ni lazima mapenzi hayo yanatiliwa nguvu na dalili na hoja. Kwa maana nyingine ni lazima kuwafuata watu hawa. Kwa sababu yule anayempenda mtu basi humfuata na kumwigiliza. Anayedai kuwapenda ilihali anaenda kinyume nao inapokuja katika ´Aqiydah, Shari´ah na mfumo madai yake si sahihi. Kigezo hichi kimetajwa na wanazuoni kama vile Ibn Taymiyyah na wengineo. Yule anayedai kuwapenda watu basi ni lazima kuwafuata watu hao kiasi cha uwezo wake. Hii ndio dalili ya mapenzi na inapelekea kufufuliwa pamoja nao. Lakini mwenye kusema kuwa eti anampenda Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakati huohuo anaenda kinyume naye katika ´Aqiydah, Shari´ah na mfumo wa ulinganizi, basi anapaswa kuikagua nafsi yake kabla hajachelewa. Mtu huvuna kile alichopanda. Kila tendo la jinao lina malipo yake mbele ya Allaah na Mola wako hamdhulumu yeyote. Akienda nao sambamba katika baadhi ya mambo na akaenda kinyume nao katika mengine ni kasoro ambayo anapaswa kupingana nayo. Kwa sababu ni lazima kwa kila mtu kuifanyia kazi Shari´ah ya Allaah kwa njia sahihi.
[1] al-Bukhaariy (6168) na Muslim (2640).
- Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 110-111
- Imechapishwa: 13/05/2026
Kila ambaye atafuata njia ya watu hawa wema ni miongoni mwao na atafufuliwa pamoja nao siku ya Qiyaamah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtu atakuwa pamoja na yule anayempenda.”[1]
Yule anayempenda Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake watukufu na maimamu wa elimu katike vile vizazi vyema atafufuliwa pamoja nao. Nawapongeza wale wanaofuata ´Aqiydah na Shari´ah ya Mtume mteule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na amekula khasa yule mwenye kwenda kinyume na Sunnah na Ahl-us-Sunnah!
Haitoshi kudai tu kumpenda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na wale waliokuja baada yao. Ni lazima mapenzi hayo yanatiliwa nguvu na dalili na hoja. Kwa maana nyingine ni lazima kuwafuata watu hawa. Kwa sababu yule anayempenda mtu basi humfuata na kumwigiliza. Anayedai kuwapenda ilihali anaenda kinyume nao inapokuja katika ´Aqiydah, Shari´ah na mfumo madai yake si sahihi. Kigezo hichi kimetajwa na wanazuoni kama vile Ibn Taymiyyah na wengineo. Yule anayedai kuwapenda watu basi ni lazima kuwafuata watu hao kiasi cha uwezo wake. Hii ndio dalili ya mapenzi na inapelekea kufufuliwa pamoja nao. Lakini mwenye kusema kuwa eti anampenda Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakati huohuo anaenda kinyume naye katika ´Aqiydah, Shari´ah na mfumo wa ulinganizi, basi anapaswa kuikagua nafsi yake kabla hajachelewa. Mtu huvuna kile alichopanda. Kila tendo la jinao lina malipo yake mbele ya Allaah na Mola wako hamdhulumu yeyote. Akienda nao sambamba katika baadhi ya mambo na akaenda kinyume nao katika mengine ni kasoro ambayo anapaswa kupingana nayo. Kwa sababu ni lazima kwa kila mtu kuifanyia kazi Shari´ah ya Allaah kwa njia sahihi.
[1] al-Bukhaariy (6168) na Muslim (2640).
Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 110-111
Imechapishwa: 13/05/2026
https://firqatunnajia.com/40-mapenzi-ya-kweli-kwa-mtume-na-salaf/