Imaam Ahmad bin Hanbal (Rahimahu Allaah) amesema:

Watu bora baada ya watu hawa ni Maswahabah wengine wote wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam); karne ambayo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametumilizwa kwao. Wale waliotangamana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakamuona kwa macho (hata kama ni kwa muda mchache), wakamsikia na wakamuamini ni wabora kuliko wale waliokuja baadaye ambao hawakumuona hata kama watatenda matendo mazuri yote.

MAELEZO

Hawa ndio watu wa karne ya kwanza. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema juu yao:

“Wabora wenu ni karne yangu, kisha wale watakaofuata, kisha wale watakaofuata.”[1]

Karne mbili au tatu baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) vinaitwa vizazi Vyema. Miongoni mwao ni kile kizazi ambacho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitumwa kwao na karne mbili au tatu baada yake. Msimulizi alisema:

“Sijui kama baada ya kutaja karne yake alitaka karne mbili au tatu.”

Hivi ndio vizazi bora kutokana ubora walionao. Kizazi cha kwanza ni cha Maswahabah. Walikuwa na matendo matukufu na kupambana jihaad katika njia ya Allaah wakati ambapo maadui wote walikuwa dhidi ya waislamu na ulinganizi wa Uislamu. Kutokana na jihaad yao, ulingano na matendo yao Allaah akanusuru ulinganizi wa Kiislamu. Baada ya kunafuata kizazi ambacho nacho kina ubora na kheri. Karne ya pili na karne ya tatu walikuwa na elimu iliobobea. Waliandika Sunnah, wakaeneza elimu, wakafunza Qur-aan, kufunza Sunnah na kupambana jihaad katika njia ya Allaah.

[1] al-Bukhaariy (2651) na Muslim (2535).

  • Muhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 110
  • Imechapishwa: 13/05/2026