Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa nguo ambayo iko wazi kwa mbele, kwa nyuma na kwa ubavu kwa namna ya kwamba muundi wa mwanamke unaonekana. Hoja yao ni kwamba wako baina ya wanawake tu.

Jibu: Ni wajibu kwa mwanamke kujisitiri kwa nguo inayositiri. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ametaja namna ambavo wanawake wa kiswahabah walikuwa wakivaa kanzu zenye kuwafunika kuanzia kwenye viganja vya mikono mpaka kwenye nyayo za miguu, kuanzia viwiko vya mikono hadi miguuni. Mipasuko hii inaonyesha miundi na pengine huko m bele jambo likapea na kwenda mbali zaidi ya hivo. Ni wajibu kwa mwanamke kujiheshimu ipasavyo ili asiingie ndani ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kuna watu aina mbili wa Motoni sijawaona: wanaume walio na bakora kama mkia wa ng´ombe ambazo wanawapiga kwazo watu, na wanawake waliovaa vibaya, uchi, waliopinda na wanawapindisha wengine. Vichwa vyao ni kama nundu ya ngamia. Hawatoingia Peponi na wala hawatonusa harufu yake. Harufu yake inapatikana umbali wa kadhaa na kadhaa.”[1]

[1] Muslim (2128) na Ahmad (2/356).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/272)
  • Imechapishwa: 13/05/2026