Kutoka katika I´tikaaf kwa ajili ya kwenda kuwatembelea wazazi wagonjwa au kuwazika

Swali: Akiugua mama au baba au akafa mmoja wao ambapo yule mwenye kukaa I´tikaaf akatoka kwa ajili ya kusindikiza jeneza au kwa ajili ya kuwatembelea I´tikaaf inakatika kwa kitendo hicho ikiwa hakuweka sharti kabla?

Jibu: Maoni ya karibu – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba inakatika. I´tikaaf ni kule mtu kulazimiana na msikiti kwa ajili ya kumtii Allaah (Jalla wa ´Alaa) na mtu asitoke isipokuwa kwa haja yake. Haja ya mtu ni kama vile kukidhi haja ndogo, haja kubwa na jambo ambalo analazimika kulifanya. Ni ´ibaadah inayopendeza. Haina neno akiikata kwa ajili ya kuwatembelea wazazi. Jambo ni lenye wasaa. Ni kama ambavo mtu anakata swawm inayopendeza ikihitajika au swalah inayopendeza ikihitajika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23823/ما-الذي-ينقطع-به-الاعتكاف-في-المسجد
  • Imechapishwa: 06/05/2024